#Business

AFRIKA MASHARIKI YAKADIRIA HASARA WENYE MELI WAKISITISHA SAFARI UARABUNI

Kampuni mbali mbali za usafiri wa meli za mizigo zinazohudumia Afrika Mashariki zimetangaza usumbufu katika usambazaji wa bidhaa kufuatia vita vinavyoendelea kati ya Israeli na mshirika wake Marekani dhidi ya Iran, zikibainisha kuwa yameanzisha gharama zinazohusiana na hatari katika shughuli zao.

Katika ushauri,kampuni hizo zimetangaza kwamba zinasimamisha shughuli zote za mizigo inayokwenda Mashariki ya Kati, na meli ambazo tayari ziko katika maeneo yaliyoathiriwa zimesimamisha kazi.kampuni hizo pia zimeanzisha ada za dharura zinazotokana na mgogoro unaoshuhudiwa kati ya $20 na $40 kwa kontena ya futi 20 kutokana na mabadiliko ya njia na ongezeko la gharama za usafirishaji.

Usafirishaji wa chai na kahawa nchini Kenya utacheleweshwa katika Bandari ya Mombasa huku meli zikipangwa upya. Vile vile Gharama ya bidhaa za petroli inatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa kufuatia usumbufu wa njia ya usambazaji.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *