WAJUMBE WA ODM NAIROBI WAMUIDHINISHA WINNIE ODINGA KAMA MWAKILISHI WA NAIROBI
Wajumbe wa ODM katika kaunti ya Nairobi wamemuidhinisha Winnie Odinga kuwa mwakilishi wa eneo Bunge la Kibra na jimbo la Nairobi kiujumla , hatua ambayo maafisa wa chama wanasema itafungua njia yake kuingia katika Baraza la Kitaifa la Uongozi la chama hicho.
Uamuzi huo umefikiwa wakati wa mkutano wa wajumbe wa ODM Nairobi uliofanyika katika ukumbi wa JOOF ukiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Nairobi George Aladwa na kuhudhuriwa na Winnie Odinga.
Aladwa amesema wajumbe wa Nairobi wamekubaliana kwa pamoja kumteua Winnie Odinga kama mwakilishi wao , akihusisha uamuzi huo na muundo wa juu wa uongozi wa chama hicho.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































