MVUA KUBWA KUANZA ALHAMISI
Wakenya wametahadharishwa kuhusu viwango vya juu vya mvua katika baadhi ya maeneo tya nchi kuanzia hapo kesho, idara ya utabiri wa hali ya anga ikisema mvua hiyo itanyesha kwa vipindi.
Kwa mujibu wa utabiri wake, nyanda za juu za magharibi na mashariki mwa bonde la ufa, ukanda wa Ziwa Victoria, nyanda za chini za Mashariki mwa nchi na ukanda wa pwani yatashuhudia mvua.
Idara hiyo imeonya kuhusu uwezekano wa mvua kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo hayo na kuwataka wakazi kuchukua tahadhari.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































