#Local News

RUTO ASEMA ATAZINGATIA MAENDELEO SI SIASA

Rais William Ruto amepuuza ukosoaji unaoendelea kutoka kwa viongozi wa upinzani akisema atazingatia kuwatumikia Wakenya na kutumia “asilimia moja” tu ya muda wake katika mijadala ya kisiasa.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Uwanja wa Busia katika Kaunti ya Busia County, Rais ameonyesha msimamo thabiti kufuatia siku ya malumbano ya hadhara kati ya viongozi wa serikali na wakosoaji wake.

Ruto amesema utawala wake hautavurugwa na mashambulizi ya kisiasa, akisisitiza kuwa kipaumbele chake ni utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na maendeleo ya taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *