#Local News

ODM: TUTAMPA RUTO MGOMBEA MWENZA

Wadhifa wa atakayekuwa mgombea mwenza wa Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao umeendelea kuibua gumzo, viongozi wa chama cha ODM kutoka Pwani wakitaka wadhifa huo kutengewa ODM.

Kauli za viongozi hao zinajiri huku wenzao wa UDA kutoka Mlima Kenya wakishikilia kuwa wadhifa huo utasalia mikononi mwa naibu rais wa sasa Kithure Kindiki.

Hata hivyo, ODM inapendekeza Waziri wa madini Hassan Joho kupewa wadhifa huo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *