SERIKALI YAVUNJA KIMYA CHA PASIPOTI
Maswali yameendelea kuibuka kuhusu ni kwanini serikali imechukua muda mrefu kutoa msimamo wake kuhusu taarifa za kuwapa paspoti za usafiri makamanda wa kundi la wapiganaji la RSF nchini Sudan, na badala yake kujitokeza hapo jana baada ya wiki kadhaa kukanusha taarifa hizo.
Katibu mkuu katika idara ya uhamiaji Dakta Belio Kipsang, amesema suala hilo linaangaziwa na wizara ya masuala ya kigeni, akikanusha utoaji wa stakabadhi hizo muhimu bila kutoa ufafanuzi wala maelezo yanayostahili uzito wa suala hilo.
Kulingana na wadadisi, huenda serikali ilisalia kimya ili kujiandaa na majibu maalum.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































