UPINZANI WALALAMIKIA UHABA WA KIEMS
Tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, imetakiwa kutuma vifaa vya kutosha vya kielektroniki vya kuwasajili wapiga kura, mbali na maafisa wa kutosha ili kuhakikisha kila anayehitaji kusajiliwa anafikiwa.
Ni wito uliotolewa na viongozi wa muungano wa upinzani wanaoendeleza ziara yao katika eneo la Ukambani, wakiibua madai ya uhaba wa vifaa hivyo katika mengi ya maeneo.
Aidha, wameitaka serikali kuharakisha mchakato wa utoaji vitambulisho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































