UHABA WA MAFUTA WANUKIA
Serikali imejiandaa kuwalinda wakenya dhidi ya bei ghali ya mafuta kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo unaotarajiwa kufikia katikati mwa mwezi huu, ikisema itatumia takribani shilingi bilioni 17 kutoka hazina ya udhibiti wa bei kuwakinga wakenya dhidi ya bei ya juu ila kwa kipindi kifupi.
Akiwa mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu fedha na mipango, Waziri wa fedha John Mbadi, amesema kuwa kuna mafuta ya kutosha kwa muda mfupi kutokana na matatizo ya usambazaji wa mafuta katika eneo la Mashariki ya kati.
Hata hivyo, amesema uhaba huo hautashuhudiwa kwa sasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































