AMBANI AFURAHISHWA NA USHINDI WA LEOPARDS
Kocha wa AFC Leopards, Fred Ambani, ameonyesha kuridhishwa na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Murang’a Seal katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Nyayo.
Matokeo hayo yameimarisha mbio za ubingwa kwa Leopards, yakipunguza tofauti ya pointi kati yao na vinara wa ligi, Gor Mahia, hadi pointi mbili baada ya michezo 27 ya msimu.
Baada ya nusu ya kwanza kuwa ya ushindani mkali, Leopards walipata mabao yao katika kipindi cha pili kupitia Ronald Sichenje na Hassan Beja, ushindi ambao Ambani ameueleza kuwa ulipatikana dhidi ya mpinzani aliyekuwa amejiandaa vyema.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































