#Local News

TAMASHA ZA MUZIKI: SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KAULI ZA KISIASA 

Maswali yameibuka kuhusu ukiukaji wa haki za kujieleza kupitia Sanaa, kufuatia hatua ya serikali kupiga marufuku jumbe za kisiasa katika michezo ya tamasha za kitaifa za muziki kwenye tamthilia za shule na vyuo.

Tamasha hizo za 64 za tamthilia na filamu za Kenya zinaanza leo katika kaunti ya Nyeri, baadhi ya shule zikiondolewa kwa tamasha hizo licha ya kufanya vyema katika hatua za awali, baada ya kubainika kwamba tamthilia zao zina kauli mbiu za kisiasa zilizopigwa marufuku kama vile Singapore, One Term na Two Term.

Marufuku hiyo inafuatia utata uliojiri mwaka jana kutokana na mchezo wa Echoes of War ulioandikiwa na naibu kinara wa DCP Cleophas Malala na kuwasilishwa na shule ya Butere Girls.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *