LIGI KUU YA SOKA UINGEREZA EPL YAREJEA
Ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL, itarejea wikendi hii baada ya kuchukua mapumziko ya wiki 3 kuwaruhusu wachezaji kuwajibikia timu zao za taifa na awamu ya robo fainali ya kombe la FA.
Yanayoangaziwa pakubwa ni timu kuwania nafasi za kucheza barani Ulaya msimu ujao, mbali na kinyang’anyiro kati ya Arsenal na Manchester City kuwania taji la EPL hasa baada ya Gunners kuyumba huku City wakiwika jijini.
Wanaporejea wikendi hii dhidi ya AFC Bournemouth, Arsenal watalenga kujisahaulisha masaibu ya kupoteza mataji mawili ya FA na Carabao wakati wa likizo hiyo, lengo likiwa ni kumaliza kiu cha kusubiri taji la EPL kwa zaidi ya miaka 22.
Manchester City nao watakuwa safarini kuelekea London ambako watamenyana na Chelsea.
Wakati uo huo, Arne Slot na vijana wake wa Liverpool watakuwa na shinikizo kutamatisha mkosi wa matokeo duni watakapoialika Fulham, huku pia wakilenga kufuzu nusu fainali ya kombe la klabu bingwa bara Ulaya.
Macho pia yataelekezwa kwa Tottenham kuona iwapo mkufunzi mpya Roberto De Zerbi atawaokoa dhidi ya kushushwa daraja, hali wanayokabiliana nayo kwa mara ya kwanza tangu miaka 50 iliyopita.
Mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Sunderland.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































