#Local News

SIKU YA MAANDAMANO HII HAPA

Maandamano yameratibiwa kufanyika katika maeneo mbali mbali ya nchi hii leo ambapo waandalizi wanalalamikia bei ya juu ya mafuta iliyotangazwa wiki jana na serikali.

Kupitia kauli mbiu ya Reject Fuel Prices, wakenya wanalenga kuishinikiza serikali kupunguza bei ya mafuta mbali na kuangazia gharama ya juu ya maisha ambayo imechangiwa na ongezeko la bei hizo.

Jijini Nairobi, kamanda wa polisi Issa Mohamoud ameshikilia kuwa maandamano hayo ni haramu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *