#Football #Sports

BANDARI FC YATULIZA TAHARUKI BAADA YA KISA KASARANI

Klabu ya Bandari FC imejitokeza kutuliza hali kufuatia tukio la mvutano lililoshuhudiwa katika mechi yao dhidi ya Gor Mahia uwanjani Kasarani mwishoni mwa wiki

Kocha mkuu Bernard Mwalala amekiri kuwa mwitikio wa wachezaji wake baada ya uamuzi tata wa penalti haukuwa wa kawaida akisisitiza kuwa nidhamu na heshima ni misingi muhimu ya klabu hiyo

Mwalala amesema alilazimika kuingilia kati wakati wa tukio hilo ili kupunguza mvutano na kurejesha utulivu huku akiahidi kuwa hali kama hiyo haitajirudia tena.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *