#Local News

JAJI WARSAME NDIYE CHAGUO

Rais William Ruto anatarajiwa muda wowote kumteua rasmi jaji wa mahakama ya rufaa Mohammed Warsame kuwa jaji wa mahakama ya upeo, kufuatia kuteuliwa kwake hapo jana na tume ya huduma za mahakama, JSC.

Warsame ni miongoni mwa watu 5 waliohojiwa kwa muda wa siku mbili na JSC, mahojiano yake yakiendeshwa hapo jana kabla ya kuteuliwa kwake huku tume hiyo ikisema alionyesha uwezo mkubwa wa kuwa jaji wa mahakama ya upeo.

Jaji mkuu Martha Koome ni mwenyekiti wa JSC.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *