#Football #Sports

HARAMBEE STARS YASALIA NAFASI YA 109 DUNIANI

Harambee Stars imesalia katika nafasi ya 109 kwenye viwango vya hivi karibuni vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) vilivyotolewa baada ya kukamilika kwa Kombe la Dunia.

Kenya ilicheza mechi zake za mwisho mwezi Juni dhidi ya Lesotho, ikitoka sare ya bao 1-1 kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano. Kutokana na kutocheza mechi nyingine tangu wakati huo, nafasi yake haijabadilika.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda ndiyo taifa linaloongoza kwa kushika nafasi ya 89 duniani, huku Kenya ikisalia mbele ya Tanzania, ambayo imeorodheshwa katika nafasi ya 112 kwenye viwango vya FIFA.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *