#Local News

KARUA AKATAA NAFASI YA NAIBU RAIS

Kiongozi wa chama cha People’s Liberation Party Martha Karua, amesema hatakubali kugombea nafasi ya Naibu Rais chini ya muungano wa upinzani, akisisitiza kuwa atalenga urais au kumuunga mkono atakayeteuliwa kupeperusha bendera ya muungano huo.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Karua amesema viongozi wa upinzani wamekubaliana kupata mgombea mmoja wa urais kupitia mchakato wa uteuzi utakaozingatia sheria na makubaliano ya muungano.

Aidha, Karua pia ameangazia mageuzi ambayo atayafanya iwapo atachaguliwa kama rais.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *