#Local News

MGOMO WA WAHUDUMU WA AFYA WAANZA NCHINI

Huduma za afya nchini zimeathirika baada ya maelfu ya wahudumu wa afya chini ya Muungano wa Vyama vya Afya kuanza mgomo wa kitaifa hapo jana

Mgomo huo umeanza kufuatia kumalizika kwa notisi ya siku 14 iliyotolewa Julai 6, baada ya mazungumzo kati ya vyama vya wafanyakazi, serikali ya kitaifa na serikali za kaunti kutofikia mwafaka kuhusu masuala ya kikazi.

Hatua hiyo inatarajiwa kuvuruga utoaji wa huduma katika hospitali nyingi za umma huku wahudumu wakisisitiza kuwa hawatarejea kazini hadi malalamishi yao yatakaposhughulikiwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *