#Football #Sports

MWAMUZI ANTHONY TAYLOR ASTAAFU

Mwamuzi wa Ligi Kuu ya Uingereza na Kombe la Dunia, Anthony Taylor, ametangaza kustaafu uamuzi baada ya kuhudumu kwa miaka 20, akitaja shinikizo na ukosoaji mkubwa unaowakabili waamuzi kuwa miongoni mwa sababu za uamuzi wake.

Taylor mwenye umri wa miaka 47 ameongoza jumla ya mechi 831, zikiwemo 432 za Ligi Kuu ya England, na kujijengea sifa kama mmoja wa waamuzi mashuhuri duniani.

Mchezo wake wa mwisho ulikuwa katika Kombe la Dunia ambapo Uhispania iliifunga Ureno bao 1-0, akihitimisha rasmi safari yake ndefu ya uamuzi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *