CA YAAGIZA WASAMBAZAJI WA VIFAA VYA TEHAMA KUPATA LESENI MPYA.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA) imetangaza masharti mapya ya leseni yanayowataka wanabiashara wote wanaoagiza na kusambaza vifaa vya mawasiliano kupata leseni ya Msambazaji wa Vifaa vya Mawasiliano (CED) kwani hatua hii inalenga kuimarisha udhibiti wa sekta ya mawasiliano.
Katika taarifa, mamlaka hiyo imeeleza kuwa masharti hayo mapya yanatokana na Muundo Uliofanyiwa Marekebisho wa Soko la Mawasiliano uliochapishwa katika Gazeti la Serikali kupitia Notisi Nambari 3335 ya tarehe 6 Machi, mwaka huu, kwa mujibu wa Sheria ya Habari na Mawasiliano ya Kenya.
Vile vile,Chini ya mfumo mpya, kampuni yoyote inayotaka kuagiza au kuuza kwa jumla vifaa vya mawasiliano nchini Kenya lazima kwanza ipate leseni ya CED kabla ya vifaa hivyo kuidhinishwa na mamlaka husika na kuidhinishwa kupitia mfumo wa TradeNet..
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































