#Local News

KMPDU YAONYA KUANZA MGOMO WAO RASMI

Chama cha Madaktari nchini KMPDU, kimewaelekeza madaktari katika kaunti zote 47 kuchunguza kwa makini hati zao za mishahara za mwezi wa Julai, kikionya kuwa mgomo wa kitaifa utaanza iwapo serikali za kaunti zitashindwa kutekeleza nyongeza za mishahara zilizokubaliwa chini ya Mkataba wa Makubaliano ya Pamoja ya mwaka 2017 hadi 2021.

KMPDU inasema hakuna tena sababu za  kisheria wala kiutawala zinazoweza kuhalalisha kucheleweshwa kwa utekelezaji wa viwango vipya vya mishahara ya msingi au kutotolewa kwa ratiba ya wazi ya kulipa mishahara inayodaiwa.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *