METTE: KOMBE LA CECAFA LITAINOA TUSKER
Kocha wa Tusker Julien Mette, amesema mashindano ya Kombe la CECAFA Kagame 2026 yatakuwa maandalizi muhimu kwa timu hiyo kuelekea ushiriki wake katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mabingwa wa Kombe la Mozzart Bet, Tusker, watasafiri hadi Kigali, Rwanda, wakilenga kushindania ubingwa wa ukanda huku wakitumia mashindano hayo kuimarisha utimamu wa mwili, mshikamano wa kikosi na mbinu za uchezaji.
Mette amesema Tusker ilialikwa kushiriki mashindano hayo baada ya klabu ya Al Merreikh ya Sudan kujiondoa, akieleza kuwa fursa hiyo imekuja kwa wakati mwafaka kuelekea msimu mpya na mashindano ya bara Afrika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































