#Local News

KARAURI ATANGAZA AZMA YA KUGOMBEA UGAVANA NAIROBI

Mbunge wa Kasarani, Ronald Karauri, ametangaza rasmi azma yake ya kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Akizungumza katika mkutano ulioongozwa na Rais William Ruto katika Ikulu,Karauri alitetea mpango wa Nyumba za Bei Nafuu, akisema umetoa ajira na kuboresha maisha ya wananchi wengi.

Aidha, alimkosoa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kwa kauli zake kuhusu mpango huo, akisisitiza kuwa utekelezaji wa mradi huo umeleta manufaa kwa mafundi na wakazi wengi wa jiji.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *