AMINA MARTHA KUFUNGUA KAMPENI YA NGUMI KWA KENYA KWENYE MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA
Bondia wa Kenya Amina Martha atakuwa Mkenya wa kwanza kupanda ulingoni katika Michezo ya Jumuiya ya Madola 2026 atakapokabiliana na Lauren Mackie wa uingereeza katika uzani wa bantamweight leo mjini Glasgow, Scotland.
Pambano hilo litakuwa la kwanza kwa timu ya ngumi ya Kenya katika mashindano hayo na kumpa Amina fursa ya kuendeleza mafanikio yake katika medani ya kimataifa.
Amina, ambaye pia ni mwanahabari na mtaalamu wa mawasiliano ya kidijitali, ni bingwa wa AFBC Zone Three wa mwaka 2025 na mshindi wa medali ya shaba katika Michezo ya Afrika 2024, ambapo aliandika historia kwa kuwa Mkenya wa kwanza kutwaa medali ya ngumi katika mashindano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































