CAK: TATIZO LA INTANETI KUENDELEA

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini CAK David Mugonyi amesema kwamba huenda tatizo lililopo la intaneti kutokana na kukatika kwa nyaya za chini ya bahari likachukua muda kutatuliwa.
Katika taarifa kwa vyombo vya Habari, Mugonyi amesema tatizo hilo lingalipo licha ya wahudumu wa mtandao kufanya juhudi za kuafikia muunganisho wa udhabiti kamili.
Aidha, amepongeza wahudumu wa mtandao ni kampuni za mawasiliano kwa juhudi zao za kuhakikisha uwepo wa intaneti.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































