OMBI LA RUTO KWA KI MOON
Rais William Ruto ametoa wiot kwa shirika linalotoa misaada kwa serikali na mashirika ya kibinafsi GCA kuanzisha idara ya kutoa mafunzo kuhusu uongozi katika chuo kikuu cha Naiorbi.
Katika kikao na mwenyekiti wa shirika hilo Ban KI Moon nchini Korea Kusini, ruto amesema idara hiyo itasaidia katika kutoa mafunzo maalum kuhusu mabadiliko ya hali ya anga, fedha na kawi safi.
Ruto ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Afrika wanaohudhuria kongamano nchini humo, ameipigia debe Afrika kama sauti ya kukabili mabadiliko ya hali ya anga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































