MURKOMEN ALIIDHINISHWA KUTEKELEZA MRADI WA UHAMAJI MIJINI
Baraza la Mawaziri limempa Katibu wa Wizara ya Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen idhini ya kutekeleza Mradi wa Kuboresha Uhamaji Mijini nchini Kenya (KUMIP).
Katika taarifa kwenye mtandao wa X Katibu wa Baraza la Mawaziri amesema kuwa mradi huo utahusisha kufufua Huduma ya Reli kwa Wasafiri na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mtandao mzima wa reli ya abiria wa kilomita 163 katika Eneo la Jiji la Nairobi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































