GARISSA: KORTI YAAMURU SERIKALI IWAFIDIE WAATHIRIWA
Mahakama kuu imeiagiza serikali ya Kenya kulipa fidia ya shilingi milioni 441 kwa familia za wanafunzi 147 waliouawa katika shambulizi la kigaidi dhidi ya chuo kikuu cha Garissa mnamo tarehe 2 mwezi Aprili mwaka 2015.
Aidha, mahakama imeiagiza serikali kuwalipa waathiriwa wa shambulizi hilo shilingi milioni 56 kama fidia, ambao wa walipata majeraha mwilini na kisaikolojia, kila familia iliyopoteza wapendwa wao ikitarajiwa kulipwa milioni 3, nao waathiriwa wakilipwa viwango tofauti tofauti.
Kwenye kesi iliyowasilishwa mnamo mwaka 2019 na shirika la Kituo cha Sheria, jopo la majaji watatu limepata Ushahidi kwamba serikali ilifeli kutekeleza jukumu lake la kuwalinda wanafunzi na hivyo kusababisha vifo na majeraha kinyume na haki zao za kikatiba.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































