MWAMBU ATEULIWA KUONGOZA UDA BUNGOMA
Chama cha UDA kaunti ya Bungoma kimemteua aliyekuwa mbunge wa Bumula Mwambu Mabonga kuwa kuwa kaimu mwenyekiti wa chama hicho na kumfurusha mbunge wa webuye magharibi Dan Wanyama kwa tuhuma za kulemaza shughuli za chama hicho.
Wakizungumza baada ya mkutano kwenye afisi za chama hicho, wanachama hao wakiongozwa na katibu mtendaji Kiprotich Siele wamesema kwamba uamuzi huo unalenga kukiimarisha chama hicho.
Aidha, wamesema kuwa mabadiliko zaidi yanatarajiwa katika kiwango cha wadi chamani humo kweney kaunti ya Bungoma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































