#Rugby #Sports

KABRAS RFC WABEBA KIKOMBE

Kabras RFC ilinyakua taji lao la kwanza la Dala 7s kwa ushindi mnono wa 24-5 dhidi ya Menengai Oilers katika uwanja wa Mamboleo Grounds siku ya Jumapili.

Ushindi huu unaipandisha Kabras RFC hadi kileleni mwa msimamo wa jedwali la Kitaifa la msururu huu wa raga ya wachezaji saba nchini, baada ya kubeba taji la Christie 7s msimu huu.

Licha ya kushindwa, Menengai Oilers wameonyesha uthabiti, na kutinga fainali kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo mnamo 2019 na 2022.

Jackson Siketa alikuwa nyota wa mchezo kwa kufunga tri tatu huku William Mwanji akiongeza tri nyingine.

Msururu huo wa kitaifa utaendelea wikendi ijayo kukiandaliwa Kabeberi 7s katika uwanja wa RFUEA jijini Nairobi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KABRAS RFC WABEBA KIKOMBE

GOR MAHIA WALAMBISHWA VUMBI

KABRAS RFC WABEBA KIKOMBE

CHELSEA YAKANYAGWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *