ODM WAPENDEKEZA ORENGO AMRITHI RAILA
Baadhi ya viongozi wa chama cha ODM wamempendekeza gavana wa Siaya James Orengo kuwa kiongozi wa chama hicho, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga.
Katika kikao na wnahabari, viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa ODM tawi la Nairobi George Aladwa, wameutaka usimamizi wa chama hicho ambao utakutana wiki hii kuhakikisha uongozi wa chama hicho ni dhabiti.
Wenyekiti wa ODM kutoka matawi yote nchini watakongamana hapo kesho kujadili mustakabali wake, Odinga anapoendeleza kampeni za kutwaa uongozi wa bara la Afrika.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































