REAL MADRID WAMNASA DIOMANDE KWA ZAIDI YA EURO MILIONI 100
Real Madrid imefikia makubaliano na RB Leipzig ya kumsajili winga wa Ivory Coast, Yan Diomande, kwa ada inayozidi euro milioni 100.
Diomande anatarajiwa kusafiri kuelekea Madrid wiki hii kwa ajili ya vipimo vya afya na kukamilisha utiaji saini wa mkataba utakaomuweka katika klabu hiyo hadi Juni 2031.
Usajili huo unatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Real Madrid, huku Diomande akionekana kuwa mmoja wa wachezaji wenye mustakabali mkubwa katika soka la Ulaya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































