#Rugby #Sports

KCB YATWAA UBINGWA WA PRINSLOO SEVENS

KCB imetwaa ubingwa wa Prinsloo Sevens 2026 baada ya kuishinda Kabras Sugar 19-12 katika fainali iliyochezwa kwenye Nakuru Athletics Club, na kuanza vyema utetezi wa taji la Mzunguko wa Kitaifa wa Raga ya Wachezaji Saba.

Chini ya kocha Andrew Amonde, KCB ilimaliza mashindano bila kupoteza mchezo wowote. Katika hatua ya mtoano, iliichapa wenyeji Nakuru RFC kwa 19-0 kabla ya kuiondoa Kenya Harlequin kwa ushindi wa 24-12 na kufuzu fainali.

KCB pia iling’ara katika hatua ya makundi kwa kuwashinda Nondescripts 29-12NYS Spades kwa 14-0, na Catholic Monks kwa 25-5, na hivyo kumaliza kileleni mwa kundi lao kabla ya kutwaa ubingwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *