VIONGOZI WA ODM WAMTAKA OPARANYA AWE NAIBU RAIS
Baadhi ya viongozi wa ODM wamekitaka chama hicho kuhakikisha kinapata nafasi ya Naibu Rais katika mazungumzo yake ya kisiasa na UDA, huku wakimuunga mkono Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya kuwa mgombea mwenza wa Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Wakizungumza katika eneo la Malava, Kaunti ya Kakamega, viongozi hao wamesema uungwaji mkono wa ODM kwa azma ya Rais Ruto ya kutetea urais utategemea chama hicho kupata nafasi ya Naibu Rais.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































