#Football #Sports

STARLETS YAPIGWA 4-0 NA MOROCCO WAFCON

Harambee Starlets ilianza vibaya kampeni yake ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 baada ya kuchapwa mabao 4-0 na wenyeji Morocco katika mechi ya Kundi A iliyochezwa mjini Rabat.

Wakipewa hamasa na mashabiki wao katika Uwanja wa Moulay El Hassan, morocco walitawala mchezo tangu dakika za mwanzo na kuonyesha ubora wao, huku Kenya ikishindwa kuhimili presha hiyo katika mechi yake ya kwanza ya mashindano hayo baada ya miaka kumi.

Hata hivyo, Starlets ilipata nafasi ya mapema kupitia mshambuliaji Tereza Engesha, ambaye shuti lake liligonga mwamba wa lango. Baada ya nafasi hiyo kupotea, Morocco ilichukua udhibiti wa mchezo na kufunga mabao manne yaliyowapa ushindi mnono.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *