WAHADHIRI WATISHIA KUVURUGA SULUHU
Mgomo wa wahadhiri umeingia siku ya 21 hii leo huku wahadhiri wakishinikilia kuwa hawatarejea kazini hadi serikali itakapowalipa deni lao la shilingi bilioni 7.9 walizokubaliana kwenye mkataba wa maelewano yaani CBA ya mwaka wa 2017-21.
Wahadhiri hao walioandamana hapo jana hadi katika majengo ya bunge, wizara ya elimu na ile ya fedha, wamesema mkutano uliopangwa hii leo kusaka suluhu utasambaratishwa iwapo serikali itapendekeza mabadiliko kufanywa.
Wanafunzi pia wameonya kujiunga na wahadhiri wao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































