MALEMA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO
Kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema amehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kupatikana na hatia ya umiliki wa bunduki kinyume cha sheria na ufyatuaji mbele ya umma.
Wakili wa Malema amesema kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo ili kumzuia kiongozi huyo wa EFF kutupwa gerezani.
Mwaka Uliopita Malema alihukumiwa kwa makosa Matano yakiwemo umiliki wa bunduki kinyume cha sheria pamoja na risasi, ufyatuaji wa bunduki mbele ya umma, pamoja na kuhatarisha maisha.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































