TAHADHARI KWA WANAO VUKA BARABARA BADALA YA KUTUMIA KIVUKIO
Watu 35 wamekamatwa katika eneo la Buruburu jijini Nairobi kwa madai ya kutotumia daraja maalumu la kuvukia barabara ikiwa ni hatua ya Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani NTSA ya kudhibiti mienendo hatari ya wanaotembea kwa miguu.
Aidha NTSA imesema operesheni hiyo inalenga watu wanaovuka barabara katika makutano ya Buruburu bila kutumia daraja kitendo ambacho mamlaka hiyo inasema kinahatarisha maisha na kuvuruga mtiririko wa magari.
Kwa mujibu wa NTSA washukiwa wote 35 watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili kuhusiana na ukiukaji huo wa sheria za usalama barabarani.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































