WANAOUNGA MKONO SERIKALI JUMUISHI WAONGEZEKA
Uungwaji mkono wa serikali jumuishi kati ya ODM na UDA uliongezeka maradufu katika kipindi cha miezi 6 iliyopita, ukipanda kutoka asilimia 22 mwezi Mei hadi asilimia 44 kufikia mwezi Novemba mwaka huu.
Haya nu kulingana na utafiti wa shirika la TIFA, uliolenga kupata maoni kuhusu ushirikiano wa kisiasa kati ya Rais William Ruto na aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga.
Kwenye utafiti huo, idadi ya wanaopinga ushirikiano huo imeshuka kutoka asilimia 64 mwezi Agosti hadi asilimia 48 mwezi jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































