WAITITU, MKEWE MAHAKAMANI
Aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu ambaye anatumikia kifungo cha miaka 12 gerezani kwa kosa la ufisadi unaohusisha shilingi milioni 588, anatarajiwa kufika mahakamani leo na mkewe Susan Wangari kuhusiana na kesi inayotaka mali yao kutwaliwa.
Maagizo ya kufika mahakamani yalitolewa na jaji wa mahakama ya kupambana na ufisadi Nixon Sifuna, baada yao kukosa kufika mahakamani wakati wa kutolewa kwa uamuzi katika kesi ambapo tume ya EACC inataka mali yao yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.9 itwaliwe.
Kulingana na EACC, mali hiyo vikiwemo viwanja katika maeneo mbali mbali, ilipatikana kwa njia za ufisadi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































