#Football #Sports

ARSENAL YATIA BREKI REKODI YA VILLA

Klabu ya Arsenal ilitamatisha rekodi ya ushindi wa mechi 11 mfululizo wa Aston Villa kwa kuicharaza mabao 4-1 katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza EPL jana usiku huku Chelsea na Manchester United wakipoteza fursa ya kuingia top 4.

Mechi hiyo ilikuwa ya Arsenal kulipiza kichapo cha pekee katika mechi 25 kwenye mashindano yote ilichopokezwa na Aston Villa mapema mwezi huu, kwa sasa wakishikilia kikikiki usukani wa ligi hiyo.

Baada ya kukaza kwa dakika 45 za ufunguzi na kupoteza nafasi za wazi kupitia kwa Ollie Watkins, Villa walisambaratika katika kipindi cha pili na kuruhusu mabao 4 yaliyofungwa na Gabriel Magalhaes, Martin Zubimendi, Leandro Trossard na Gabriel Jesus, kabla ya Watkins kuwafuta machozi Villa dakika za majeruhi.

Kwa sasa Arsenal wanaongoza kwa pointi 45 baada ya mechi 19, wakiwa mbele ya Manchester City na pointi 5 ingawa City wana fursa ya kupunguza mwanya huo watakapovaana na Sunderland hapo kesho.

Katika matokeo mengine, Wolves walipata pointi yao ya 3 ya msimu katika sare ya bao 1 dhidi ya Manchester United ugani Old Trafford, Chelsea nao wakisalia na ushindi mmoja pekee katika mechi 7 za ligi kufuatia sare ya mabao 2 mikononi mwa Bournemouth.

United wanasalia katika nafasi ya 6, pointi 2 nje ya top 4 baada ya kupoteza nafasi ya kipekee dhidi ya Wolves

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

ARSENAL YATIA BREKI REKODI YA VILLA

TANZANIA WAINGIA HATUA YA MWONDOANO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *