POLISI WAIMARISHA KIKOSI
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini KPL Police FC, wamewasajili wachezaji 3 raia wa kigeni ili kuimarisha kikosi chake katikia juhudi za kutetea taji hilo ligi inapoingia katika mkondo wa mwisho.
Watatu hao ni Yves Koutiama wa Burkina Faso aliyeshiriki dimba la CHAN mwaka jana hapa nchini, kiungo mwenye uwezo wa kusakata nafasi mbali mbali Ernest Malonga na beki Bowamba Jacques, wote wa timu ya taifa ya Kongo Brazzaville.
Polisi wanatetea taji lao wakiwa katika nfasi ya 6 kwa pointi 22 baada ya mechi 13.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































