MPASUKO ZAIDI ODM
Tofauti za kisiasa zimeendelea kujitokeza katika chama cha ODM hasa kuhusiana na ushirikiano wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao, kinara wa chama hicho Oburu Oginga akisisitiza kuwa ODM itafanya mazungumzo na UDA ili kubuni muungano wa kisiasa.
Hata hivyo, kundi la viongozi likiongozwa na gavana wa Siaya James Orengo na katibu mkuu Edwin Sifuna, wamekariri kuwa mkataba wa maelewano ya kisiasa kati ya kinara mwanzilishi Raila Odinga na Rais William Ruto yanakamilika mwaka ujao.
Oburu amesisitiza kuwa hakuna viongozi watakaofurushwa chamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































