MIGORI YOUTH WASALIA KWENYE USAKANI NSL
Migori Youth walidumisha uongozi wao wa ligi ya divisheni ya pili, National Super League, NSL, licha ya sare ya kutofungana dhidi ya Soy United hapo jana.
Sare hiyo iliwafikishia pointi 37, sawa na Mombasa United walioandikisha ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Kabatini Youth.
Hayo yakijiri, Soy United walidumisha rekodi yao ya kutopoteza mechi nyumbani msimu huu, wakiwa wameandikisha ushindi katika mechi 8 na kutoa sare 2.
Klabu ya MOFA inayohusishwa na mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga, inasalia katika nafasi ya 3 kwa pointi 35 huku Fortune Sacco wakishikilia nafasi ya 4 kwa pointi 32.
Kwingineko, Vihiga United waliirundikia Kibera Black Stars masaibu zaidi kwa kichapo cha mabao 2-1, ingawa ushindi huo haukuwawezesha kuondoka mkiani.
Klabu hiyo inasalia kwenye basement ya NSL, wakiwa na pointi 12 pekee.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































