#Local News

MURKOMEN AZINDUA USAJILI MKUBWA WA VITAMBULISHO WEST POKOT

Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amezindua zoezi la usajili mkubwa wa watu ili kupata vitambulisho vya kitaifa katika Kaunti ya West Pokot.

Akizungumza Kapenguria, Murkomen amesema zoezi hilo litafanyika kwa pamoja katika kaunti za West Pokot, Turkana na Elgeyo Marakwet ili kuziba mapengo ya muda mrefu ya usajili wa raia.

Murkomen amebainisha kuwa kwa miaka mingi wakazi wa maeneo ya wafugaji wamekosa vitambulisho vya kitaifa, hali iliyowazuia kupata huduma muhimu za serikali, akisema zoezi hilo linalenga kurekebisha changamoto hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *