#Football #Sports

NAIROBI UNITED KUMKOSA KIUNGO WAKE

Mabingwa watetezi wa taji la FKF CUP, Nairobi United, watakosa huduma za kiungo wake Michael Karamor kutokana na jeraha wanapojiandaa kwa mechi ya leo dhidi ya APS Bomet.

Mkufunzi mkuu wa Naibois Godfrey Oduor maarufu kama Solo, amesema mabingwa hao wana hamu ya kujikung’uta vumbi kutokana na matokeo duni katika mechi za dimba la mashirikisho ya soka chini ya CAF, ambako wamepoteza mechi zote 4 walizocheza na kubakia na mechi 2 katika awamu ya makundi.

Oduor amekiri kuwa mrundiko wa mechi imekuwa changamoto, ila angali na matumaini kwamba kikosi chake kitajikomboa.

Katika mechi hizo za CAF Confederations, Nairobi United wamefungwa mabao 7 na kujibu mara moja pekee katika Group B, kwenye mechi ambazo wamepoteza dhidi ya Azam mara 2, AS Maniema na Wydad Casablanca.

Kwa sasa wamerejea nchini kutoka Tanzania wakijiandaa kwa mechi ya leo dhidi ya APS Bomet katika uwanja wa Nyayo 3pm.

Limbukeni hao wa KPL wanashikilia nafasi ya 10 kwa pointi 25, 15 nyuma ya viongozi Gor Mahia ambao wamesakata mechi 19, nao Naibois wakiwa wamesakata mechi 16.

Bomet wako katika nafasi ya 17 wakiwa na pointi 15 baada ya mechi 18, na wataingia uwanjani leo kusaka ushindi wa kwanza tangu kuanza kwa mwaka huu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

NAIROBI UNITED KUMKOSA KIUNGO WAKE

BUSIA KWENYE DARUBINI YA EACC

NAIROBI UNITED KUMKOSA KIUNGO WAKE

KIPKOSGEI BINGWA WA DUNIA RASMI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *