CHARLES KANJAMA RAIS MPYA LSK
Jumbe za kongole zimeendelea kumiminika kufuatia ushindi wa wakili Charles Kanjama kwenye uchaguzi wa urais wa chama cha wanasheria nchini LSK, ili kuchukua usukani kutoka kwa rais anayeondoka Faith Odhiambo.
Miongoni mwa waliompongeza kwa ushindi wa uchaguzi uliofanywa hapo jana ni kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, Waziri wa afya Aden Duale, Odhiambo na aliyekuwa mshindani wake Mwaura Kabata.
Kanjama aliibuka mshindi baada ya kujizolea kura 3,728, akafuatia na Peter Wanyama kwa kura 2,616 huku makamu wa sasa wa Rais wa LSK Mwaura Kabata akimaliza wa mwisho akiwa na kura 2,086.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































