WANDAYI ATETEA KUJIHUSISHA NA SERIKALI
Waziri wa kawi Opiyo Wandayi, ametetea kujihusisha kwake na shughuli za kisiasa nchini licha ya ukosoaji kutokana na wadhifa wake serikalini, akisema amekuwa akitumia majukwaa hayo kuwaeleza wakenya kuhusu utendakazi wa serikali.
Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Wandayi amepuzilia mbali kwamba hatua hiyo ni sawa na kampeni za mapema za kumpigia debe rais William Ruto kuchaguliwa kwa muhula wa pili.
Amekariri kuwa jukumu lake ni kuweka wazi mafanikio ya serikali kwa umma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































