BEI YA YAI YAPANDA HADI 20% KUFUATIA KUPANDA KWA MALISHO
Bei ya mayai ya kuku jijini Nairobi imepanda hadi asilimia 20 katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, ikichangiwa na kupanda kwa gharama za malisho na mahitaji ya msimu. Yai katika mashamba mengi jijini Nairobi inauzwa kati ya Ksh15 na Ksh18.
Kufuatia ripoti ni kuwa, bei za reja reja sasa ni kati ya Ksh450 hadi Ksh480 kwa trei moja, huku maduka makubwa makubwa yakitoza kati ya Ksh575 na Ksh604, hadi 30% juu kuliko bei za mitaani. Timothy Mulwa, mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa Kuku nchini, amehusisha ongezeko hilo na shinikizo la gharama za uzalishaji, uhaba wa malisho, na vikwazo vya usambazaji wa kikanda.
Tarehe 16 mwezi huu watengenezaji wa malisho ya kuku waliongeza bei ya Layers Mash kwa Ksh100 na kubainika kuwa Malisho huchangia 85-90% ya gharama za uzalishaji wa mayai, hivyo kupanda kokote kule huathiri moja kwa moja bei za mayai, ambayo sasa ni wastani wa Ksh400 kwa trei. Uchunguzi wa Mamlaka ya Ushindani wa Kenya umegundua kuwa bei ya malisho ya mifugo ni 42-54% juu kuliko Afrika Kusini na Brazili.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































