#Football #Sports

KOCHA WA LEVERKUSEN AHOJI MBINU ZA ARSENAL KWENYE MIPIRA YA KONA

Kocha wa Bayer Leverkusen Kasper Hjulmand amehoji uhalali wa mbinu za mipira ya set – piece zinazotumiwa na Arsenal kabla ya mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa hii leo nchini Ujerumani.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari Hjulmand ameuliza iwapo kuziba wapinzani wakati wa mipira ya kona kunafaa kuruhusiwa, hasa ikizingatiwa kuwa mbinu hizo zimekuwa na ushawishi mkubwa katika mchezo wa kisasa.

Timu ya Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta kwa sasa inaongoza Ligi Kuu ya Uingereza, mafanikio ambayo kwa kiasi kikubwa yametokana na uwezo wao mkubwa wa kufunga mabao kupitia mipira ya kona au set-piece.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *