#Local News

POLISI WACHUNGUZA MIILI 14 KWENYE KABURI LA PAMOJA

Maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai DCI wanaendelea kutegua kitendawili kuhusu ni vipi miili 14 isiyojulikana ilizikwa katika kaburi moja eneo la Makaburini kaunti ya Kericho Ijumaa asubuhi.

Kwa mujibu wa wapelelezi, walipata taarifa kutoka kwa vijana 2 wa kurandaranda mitaani wanaodai watu 3 walifika eneo hilo Ahamisi na kufanya mazungumzo na usimamizi wa makaburi hayo, kabla ya kurejea Ijumaa na miili na kuwashirikisha vijana hao katika kuchimba kaburi hilo.

Serikali ya kaunti hiyo imekana kuhusika na tukio hilo huku wakazi wakitaka kuwafahamu waathiriwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *